Skip to content
Back to News

Wizara ya Elimu ahudhuria Kongamano la CHAKAMA

Posted on Aug 09,2026 by kisii-university
NEWS
...

Katibu wa Baraza la Mawaziri anayesimamia Wizara ya Elimu, Mhe. Julius Migos Ogamba, EBS, leo alihudhuria Kongamano la CHAKAMA linaloendelea katika Chuo Kikuu cha Kisii, ambapo alitoa ujumbe uliowatia matumaini mapya washiriki kuhusu mustakabali wa lugha ya Kiswahili. Hotuba yake ilisisitiza nafasi muhimu ya Kiswahili kama lugha inayotuunganisha, hazina ya urithi wetu wa kitamaduni, na lugha hai inayoendelea kukua na kuendana na mabadiliko ya ulimwengu. Wakati wasomi, walimu, watafiti na wapenzi wa lugha wanapokutana kujadili na kuunda mustakabali wake, kongamano hili linaendelea kudhihirisha dhamira yetu ya pamoja ya kuikuza na kuiendeleza lugha ya Kiswahili kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo. Kwa pamoja, tunaadhimisha maendeleo yake, tunakumbatia mageuzi yake, na kuendeleza nafasi yake ya kudumu katika elimu, utafiti na jamii.


Kisii University Support
close
send