Event Details:
Chuo Kikuu cha Kisii kinajivunia kuwa mwenyeji wa Mkutano wa CHAKAMA 2026, utakaofanyika hapa chuoni mwezi ujao. Jiandae kushuhudia mkusanyiko wa wasomi, watafiti na wadau mashuhuri wa lugha ya Kiswahili wakijadili njia bora za kuiendeleza lugha ya Kiswahili katika karne ya ishirini na moja na kuimarisha mchango wake katika elimu, utafiti, teknolojia na maendeleo ya jamii. Karibu tuungane katika kongamano hili muhimu linalolenga kuinua hadhi na thamani ya Kiswahili katika ngazi za kitaifa na kimataifa.